RSS

Daily Archives: June 13, 2012

Taxation of Benefit In kind – Tanzania Income Tax Law

Kuna Mtu aliniuliza swali, amepewa nyumba ya kuishi pamoja na gari vya kampuni. Kila mwezi wanamkata kodi inajumuishwa kwenye PAYE haelewi kwa nini;

Benefit In kind inatokea pale muajiri anapofanya malipo kwa mahitaji binafsi ya muajiriwa kwa kumpatia bidhaa au huduma. (sio kwa kumpa pesa). Mfano ni Muajiri kumpatia muajiriwa Nyumba, kulipia ada za watoto wa muajiriwa,gari au kumpatia bidhaa au huduma bure au kwa bei ya chini.

Kuthaminisha kodi ya benefit in kind.

kwa ujumla kiwango cha benefit in kind kinapatikana kwa kulinganisha ile huduma uliyopatiwa na thamani yake kwenye soko. Kwa maana nyingine kama muajiri asingempa nyumba angeilipia kiasi gani?

Sheria ya Kodi tanzania inatoa maelekezo ya jumla ya kiasi cha pesa inayotakiwa kukatwa kodi kwa kupewa gari, Nyumba na Mikopo nafuu inayotokewa na kampuni kwa wafanyakazi wake.

Mfano wa Kuthaminisha Gari:  hii inategemea na saizi ya injini na umri wa gari. kiasi cha malipo kwa mwaka unagawa kwa miezi 12 na kukiongeza kwenye Taxable income of employment ya mwezi. ANGALIA CHATI CHINI.

Natumaini rafiki  umepata mwanga kwa ile kodi unayokatwa ya gari! kwa mifano zaidi ya jinsi ya kupata thamani ya riba kwa mikopo na nyumba tembelea tovuti ya TRA.

SAIZI YA INJINI YA GARI

KIASI   CHA MALIPO KWA MWAKA

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX GARI CHINI YA MIAKA MITANO GARI ZAIDI YA MIAKA MITANO
ISIYOZIDI 1000CC SHS. 250,000 SHS. 125,000
ZAIDI YA 1000CC LAKINI ISIYOZIDI 2000CC SHS. 500,000 SHS. 250,000
ZAIDI YA 2000CC LAKINI ISIYOZIDI 3000CC SHS. 1,000,000 SHS. 500,000 
JUU YA 3000CC SHS. 1,500,000 SHS. 750,000
About these ads
 

Tags: , , ,

 
Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 3,695 other followers

%d bloggers like this: